Test Index

KJSEA Kiswahili 2025 Paper 1

Show Para  Hide Para 
Question Numbers: 7-12
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 7 hadi la 12.
Zakaria alikutana na Kiberenge njiani. “Unaenda wapi?” Kiberenge alimuuliza Zakaria. “Hakuna hata salamu bwana?” Zakaria alimuuliza Kiberenge.
“Sina muda wa salamu. Nachelewa. Nataka kwenda kupanga meza zangu. Wateja wangu wanakaribia kutoka kazini. Kwanza, naomba univunjie noti hii.” Kiberenge alisema akiwa na haraka huku akimpatia Zakaria noti ya mia tano. Zakaria aliwaza na kuwazua. Hakujua amvunjie Kiberenge pesa au la. Hakumwamini Kiberenge hata kiduchu. Alimfahamu Kiberenge ndani nje. Kiberenge hakuwa mtu mwenye maadili. Alitumia kila fursa aliyopata kuwalaghai watu.
“Haidhuru!” Zakaria alijisemea na kumpa Kiberenge pesa alizohitaji. Kiberenge alizipokea pesa hizo huku akicheka na kutoa gego la mwisho.
Haukupita muda mrefu, Zakaria akafika dukani akiwa na haja ya kununua bidhaa. Alishangaa alipoambiwa kuwa pesa alizokuwa nazo zilikuwa bandia. Alirudisha mawazo nyuma na kusema, “Ala! Kumbe Kiberenge amenichezea. Sawa tu. Leo atampata pwaguzi.” Zakaria alifululiza moja kwa moja hadi mahali ambapo Kiberenge alichezeshea watu kamari. Alitumaini kuwa angempata kwani mara nyingi alikuwa akijificha asikamatwe na askari kanzu.
Zakaria alimkuta Kiberenge akiwashawishi wapita njia kucheza kamari. Aliwaita kwa sauti, “Njooni magwiji. Haraka yako ndio bahati yako. Hapa pesa zako zitazaa pacha.”
Zakaria alijibanza pembeni na kutafuta kwenye mtandao nambari ya kituo cha polisi kilichokuwa karibu. Aliipata na kuwataarifu kuhusu uhuni wa Kiberenge. Polisi walimshauri Zakaria kujidai kuwa alitaka kucheza kamari. Walimwambia atumie pesa ghushi alizopewa na Kiberenge. Zakaria alifululiza kwenda kucheza kamari kama alivyoshauriwa.
Kiberenge alimkaribisha Zakaria kwa mikono miwili. Zakaria naye hakusita; alianza kucheza mara moja kwa pesa bandia. “Hahaha! umeliwa. Wajinga ndio waliwao. Wekelea pesa zaidi ili ukomboe zilizopotea.” Kiberenge alisema huku akicheka kama fisi.
Kicheko cha Kiberenge kiligeuka kilio askari kanzu walipowasili wakiandamana na askari polisi. Askari hawa waliwazingira Kiberenge na wachezaji kamari wenzake. Zakaria alisimama kando tu na kujionea sinema.
© africaexams.com
Question : 11
Total: 43
Go to Question:
Advertisements