Test Index

KJSEA Kiswahili 2025 Paper 1

Show Para  Hide Para 
Question Numbers: 13-17
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 13 hadi la 17.
Haki ndio msingi wa mahitaji yote ya kila mtu. Mahitaji hayo ni kama vile: lishe bora, mavazi, malazi na elimu. Swali ni je, ni nani anayefaa kuwatimizia watu haki zao?
Watu tofauti hupata haki zao kupitia njia mbalimbali. Watoto kwa mfano hutimiziwa haki zao na wazazi, walezi au walimu wao. Kwa upande mwingine, wakongwe hutimiziwa mahitaji yao na wana wao na jamii kwa jumla.
Kunayo mambo mengi ambayo huathiri upataji wa haki za kibinadamu. Mambo hayo ni kama vile sheria na sera za jamii fulani. Jamii inayowajali watu wake huweka utaratibu wa kuhakikisha kuwa kila mwanajamii anapokea haki zake. Taratibu hizi huwalinda wanajamii dhidi ya dhuluma zinazotokana na ukiukaji wa haki za kibinadamu kama vile ukosefu wa elimu.
Haki za kibinadamu zinapokiukwa jamii hutamauka na kufarakana. Watu huanza kuvunja sheria na kuwadhulumu wenzao. Wengine huwatumia vibaya watu wasio na uwezo wa kiuchumi ndiposa wawatimizie angalau baadhi ya mahitaji yao.
Kumnyima mtu haki yake ni kumnyima ubinadamu wake. Ni kumfanya mtu kuwa zuzu asiyewaza chochote bali kutii analoambiwa bila kuhoji. Jamii kamili ni ile ambayo inatimiza haki za kila mwanajamii na kuzilinda kwa jino na ukucha.
© africaexams.com
Question : 14
Total: 43
Go to Question:
Advertisements