Test Index
KJSEA Kiswahili 2025 Paper 1
Show Para
Question Numbers: 21-25Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 21 hadi la 25.(Ni uwanjani. Wanafunzi wanafanya mazoezi ya mwili. Tezi na Nira wanakimbia polepole huku wakizungumza.)Tezi: (Akimsogelea.) Hali vipi Nira?Nira: Nzuri sana dada. Nawe waendelea vipi?Tezi: (Kwa furaha.) __21__. Ninaendelea kufanya mazoezi. Si unajua ni wakati wa matayarisho ya michuano ya futiboli? Timu yetu inajikaza kisabuni. Unajua, ajizi ni ...Nira: (Akidakia.) Nyumba ya njaa, eti. Hata sisi tunajikakamua.Tezi: (Akihema.) Hapo sawa mwenzangu! Mwaka jana tulinyakua kombe. Tunatumai mwaka huu pia tutalileta kwetu. Wavulana wote wameamua liwe liwalo, ushindi utabaki kwetu.Nira: Hali kadhalika, kwa upande wa timu yetu, mabanati hawalali. Tumeamua kuwa sharti tulinyakue kombe mwaka huu. Mwaka jana lilitupita.Tezi: (Akipunguza mwendo.) Wacha nipumue kidogo. Nimekimbia kwa muda mrefu; moyo wangu unadunda. Nikiendelea hivi nitaanguka.Nira: (Akisimama.) __24__. Hakika hata mimi ninahitaji kupumzika sasa. Kwaheri. Tutaonana kesho tena.Tezi: (Akimtazama.) Nami nitakufuata punde.(Wanaagana.)
© africaexams.com
Question : 24
Total: 43
Go to Question: