Test Index

KJSEA Kiswahili 2025 Paper 1

Show Para  Hide Para 
Question Numbers: 1-6
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 1 hadi la 6.
Sonita alitembea halahala kuelekea nyumbani kutoka shuleni. Alikuwa ameagana na wanafunzi wenzake na kila mtu akashika njia ya kwao. Mwendo wa kutoka mahali alipokuwa hadi kwao haukuwa mrefu. Sonita alitamani kufika nyumbani apumzike kwani alikuwa amechoka. Siku hiyo, alikuwa ameshiriki michezo shuleni. Ghafla bin vuu mawazo ya Sonita yalitekwa na sauti ya mtoto mchanga.
“Ala! Sauti ya mtoto? Mtoto anafanya nini peke yake kando ya barabara?” Maswali haya na mengine mengi yalimjia Sonita kwa wakati mmoja.
Sonita alinyatia na kuchungulia ilikotoka sauti hiyo. Alipigwa na bumbuazi kumwona mtoto mchanga amefungwafungwa kwa nguo za mararu na kutiwa ndani ya kapu kuukuu. Moyo ulimpapa. Hakujua afanye nini. Sonita aliamua kutimua mbio ili kukikwepa kioja hicho lakini kabla ya kufanya hivyo, aliyaona mengine mbele yake. Jibwa kubwa lilikuwa limelala nyuma ya kapu hilo. Lilikuwa limetulia kama maji mtungini. Sonita alidhani kuwa bila shaka azma ya jibwa hilo ilikuwa moja, kumtafuna mtoto yule. Alinyakua kapu hilo na kukimbia. Jibwa lilimwangalia kwa jicho la pembeni. Lilibaki pale likinusanusa. Sonita alifika nyumbani akihema kwa mshtuko.
“Sijui nimfanyie nini mtoto huyu? Baba na mama hawajafika nyumbani. Mtoto mwenyewe anahitaji chakula, mavazi na malazi. Afadhali niwapigie wazazi wangu simu waje haraka. Jukumu hili siliwezi peke yangu.” Sonita alisema huku akimfunika mtoto kwa blanketi ili aache kutetemeka. Mtoto mwenyewe hakulia bali alirambaramba midomo, ishara ya kutafuta riziki ya tumboni.
Wazazi wa Sonita waliwasili nyumbani haraka. Walipishana kwa sekunde tu. Aliwaeleza yote yaliyojiri. Mama alimshughulikia mtoto vyema. Alimwosha, akamfunga vizuri kwa nguo safi na kumnywesha maziwa. Mtoto alilala usingizi wa pono. Baba na Sonita nao walishika njia hadi kwenye kituo cha polisi kuripoti tukio hilo.
© africaexams.com
Question : 6
Total: 43
Go to Question:
Advertisements