Test Index

KJSEA Kiswahili 2026 Paper 1

Show Para  Hide Para 
Question Numbers: 13-17
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 13 hadi la 17.
Hapo zamani za kale wanyama waliishi kwa amani, upendo na ushirikiano chini ya mfalme wao Simba. Wote walimuenzi na kumheshimu kwa hekima yake iliyowaridhisha.
Siku moja mfalme Simba aliita mkutano wa wanyama wote na kutangaza, “Wanyama wenzangu, mimi mfalme wenu sasa nimekula chumvi nyingi. Hivi karibuni nitastaafu. Wakati umefika wa kumrithisha binti yangu kigoda cha ufalme kwa mujibu wa sheria na mila zetu. Tatizo ni moja tu! Siwezi kumkabidhi binti yangu hatamu za uongozi kabla hajaolewa. Nimewaita ili mnishike mkono katika hili, kwani palipo wengi hapaharibiki neno. Nimeona vyema niiweke nafasi wazi kwa mabarubaru wetu wote walio marika wa binti yangu walete mapendekezo ya posa. Atakayeniridhisha nitamuoza binti yangu.”
Wanyama wote walishangilia Simba alipomaliza kuzungumza. Kila mnyama barubaru aliingiwa na hamu ya kushiriki kwenye kinyang’anyiro cha posa. Mara hiyo hiyo Simba alianza kupelekewa mapendekezo. Barubaru Ndovu ndiye aliyetangulia. Alijivunia nguvu nyingi. Alikwenda kwa mfalme na kuinua miamba ya mawe na magogo mbele yake. Mfalme alisema, “Uongozi sio nguvu za mwili. Sijaridhika.” Mabarubaru walizidi kuleta posa zenye mbwembwe na maonyesho ya vichekesho lakini Simba hakuridhika.
Hatimaye barubaru Kobe alijitokeza. Alijaribu kadri ya uwezo wake kutembea asteaste kuelekea kwa mfalme kupeleka posa. Njiani alikutana na Sungura. “Unakwenda wapi rafiki yangu?” Sungura alimuuliza Kobe. “Kwa mfalme kupeleka ...” Kobe alisema kwa kusita. “Mabarubaru wote wenye kwao na vyao wameshindwa, sembuse wewe mwenda pole na mwenye haya?” Kobe hakumjibu Sungura. Alifululiza tu hadi kwa mfalme.
Alipofika, Kobe alimkabidhi Simba zawadi kwanza. Kisha akamwambia, “Baba mkwe, naomba mkono wa binti yako katika ndoa. Sina nguvu za mwili lakini hekima yangu inatosha. Nina uwezo wa kumtunza bintiyo kwa hali na mali. Nimekuwa nikifanya utafiti jinsi nitakavyohakikisha lishe bora na la kutosha kwako, binti yako na jamii yako yote kwa jumla. Kwa sasa nimeweka mitego ya kuwanasa wanyama wenye nyama teletele kama vile Ndovu na Sungura. Binti yako hatadhoofika hata siku moja!” Simba alifurahi kusikia kauli za Kobe. Kauli hizo zilimpa Simba matumaini.
“Nimekupa baraka zangu. Nitakuoza binti yangu.” Simba alisema. Binti wa Simba naye alifurahi ghaya kusikia hivyo.
© africaexams.com
Question : 16
Total: 50
Go to Question:
Advertisements