Test Index

KJSEA Kiswahili 2026 Paper 1

Show Para  Hide Para 
Question Numbers: 1-6
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 1 hadi la 6.
Katika kijiji cha Fanisi panaishi mkulima stadi anayejulikana kwa jina Mutabi. Anafuga ng’ombe, mbuzi, kuku na hata kondoo. Anawatunza wanyama wake kwa uangalifu na kuwapa lishe bora kila siku. Anafahamu fika umuhimu wa wanyama hao, kwa hivyo anajizatiti kuwahudumia kwa kila hali. Mutabi ametuzwa si mara moja kwa kuwa mkulima bora. Amekuwa akialikwa kuwahamasisha wakulima katika majukwaa mbalimbali, si kwa idhaa, si kwa mabaraza, si kwa maonyesho ya kilimo. Isitoshe, yeye hupata mialiko ya kuzungumza na wanafunzi shuleni.
Siku moja, nilipanga kumtembelea Mutabi kwake ili kujifunza mbinu bora za ufugaji wa wanyama. Nilipofika kwake alinikaribisha kwa mikono miwili. Aliniandalia chai kwa mihogo. Ilikuwa si chai ya kawaida; maziwa yalikolea vilivyo!
“Chai hii ni tamu sana,” nilimwambia mwenyeji wangu. “Imetayarishwa kwa maziwa asilia kutoka kwa ng’ombe wangu hapa hapa shambani.” Mutabi alinijibu kwa furaha.
Baada ya chai, Mutabi alinitembeza alikofugia mifugo wake. Alinifunza mengi kuhusu utunzaji wa mifugo. Alinieleza kuwa mahitaji ya mifugo ni sawa na ya binadamu. Alisema kuwa wanyama wa kufugwa wanahitaji makazi salama, chakula bora, maji safi na huduma za afya wanapougua.
Ziara yangu kwa Mutabi ilifungua ukurasa mpya katika maisha yangu kwa kuwa nilianza kilimo biashara cha mifugo. Ng’ombe wa maziwa ninaowafuga wameiletea familia yangu pato kubwa. Nina hakika kuwa nawe ukiamua kuwafuga wanyama wa nyumbani utawahudumia kwa njia ifaayo ili wawe wa manufaa kwako na kwa jamii nzima.
© africaexams.com
Question : 6
Total: 50
Go to Question:
Advertisements