Test Index
KJSEA Kiswahili 2026 Paper 1
Show Para
Question Numbers: 7-12Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 7 hadi la 12.Uadilifu ni hali ya mtu kutenda mema wakati wote. Kwa kweli, mtu mwadilifu ni yule ambaye huhakikisha kuwepo kwa haki na usawa kwa wote. Yeye huwa mwaminifu na huwajibikia majukumu yake. Mara nyingi ana msimamo thabiti katika kila jambo alifanyalo. Mtu mwadilifu ni kielelezo cha kuigwa na wanajamii wenzake.Mtu mwadilifu ana majukumu mengi katika jamii. Yeye hutambua maovu na kuyatoa hadharani. Jamii ikiwa na wanajamii wengi wanaowajibika, watashirikiana kuyakashifu maovu. Si ajabu kuwaona watu kama hawa wakitibua kashfa kubwa ambazo zingewaathiri wanajamii kwa njia hasi iwapo hazingejulikana. Kuweka wazi maovu haya huwawezesha walinda sheria kuwachunguza, kuwashtaki na kuwahukumu wahalifu. Hatua hii ni muhimu kwa kuwa husaidia kupunguza visa vya uhalifu katika jamii. Ama kweli, kinga ni bora kuliko tiba.Jamii yenye watu waadilifu hufaidika kwa njia nyingi. Mathalan miradi mbalimbali ya maendeleo huanzishwa na kukamilika kwa wakati. Ufujaji wa mali ya umma hutiwa katika kaburi la sahau. Muda wa kufanya kazi huwa umedhibitiwa, na kila hela iliyotengewa shughuli fulani hutumika inavyofaa. Kadhalika, jamii hufanya kazi kwa kujitolea na kwa ushirikiano, hivyo kuimarisha mshikamano wa kijamii. Kwa hakika jamii inayothamini maadili hukua kwa hali na mali.
© africaexams.com
Question : 9
Total: 50
Go to Question: