Test Index

KPSEA Kiswahili 2024 Paper

Show Para  Hide Para 
Question Numbers: 10-12
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Hapo zamani za kale, Kondoo na Paka walikuwa wafanyakazi wa Mbwa. Kondoo na Paka walifanya kazi kwa zamu. Walisafisha nyumba, kufua nguo na kupika. Mbwa aliwalipa kila mwisho wa mwezi kwa kazi walizofanya.
Kondoo alifanya kazi yake kwa utaratibu uliofaa. Alipika chakula kitamu kama asali na kukiandaa mezani kwa njia ya kuvutia. Mbwa alifurahia kazi ya Kondoo. Paka naye alifanya kazi yake kiholela. Mara nyingi, chakula alichopika kiliungua. Chai yake ilikuwa majimaji kwa kukosa maziwa ya kutosha. Jambo hili lilikuwa likimuudhi sana Mbwa.
Siku moja, Mbwa aliamua kumchungulia Paka akipika jikoni. Alimwona akinywa maziwa. Mbwa alirudi sebuleni na kuketi akingoja Paka aandae chai. Punde si punde, Paka alileta chai mezani. Kama kawaida, Mbwa alimuuliza Paka kuhusu maziwa aliyokuwa amemwona akinywa jikoni. Paka, alikana na kuanza kulia akimlaumu Kondoo kuwa ndiye aliyemtilia fitina kwa Mbwa. Kabla ya Kondoo kujitetea, Mbwa alitoa onyo kali kwa Paka. Alimpa siku mbili pekee ajirekebishe.
Paka aliomba msamaha kwa Mbwa. Aliahidi kufanya kazi kwa bidii na kwa uaminifu. Pia, alimwomba Kondoo msamaha kwa kumlaumu bure. Mbwa na Kondoo, walimsamehe Paka wakikumbuka kwamba mwana akinyelea paja halikatwi.
© africaexams.com
Question : 10
Total: 30
Go to Question:
Advertisements