Test Index

KPSEA Kiswahili 2024 Paper

Show Para  Hide Para 
Question Numbers: 1-5
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
(Ni shuleni, saa mbili asubuhi. Tatu na Sironi wanaelekea darasani baada ya gwaride.)
Tatu: (Akimnyooshea mkono.) Hujambo Sironi?
Sironi: Sijambo mwenzangu. Habari ya likizo fupi?
Tatu: (Akitabasamu.) __1__ rafiki yangu. Ninashukuru.
Sironi: Hongera! Nimekusikia ukiimba wimbo wa taifa vizuri na kwa ujasiri tulipokuwa tukipandisha bendera. Hata nilimwona Bwana Juma akitabasamu.
Tatu: (Akionyesha furaha.) Asante Sironi. Mimi hufurahia kuimba wimbo wa taifa kila mara ninapopata nafasi. Mwalimu alituambia kwamba tunapoimba wimbo wa taifa huwa tunajikumbusha historia ya nchi yetu.
Sironi: Kweli! Ni vyema kukumbuka jinsi mababu walivyoteseka wakipigania ukombozi wa nchi yetu.
Tatu: __2__ ! Hata rangi kwenye bendera ya taifa zinaonyesha mambo muhimu kuhusu nchi yetu. Kwa mfano, rangi nyekundu inasimamia damu iliyomwagika wakati wa vita vya ukombozi. Nayo rangi nyeupe inaonyesha amani.
Sironi: Nami najua kuwa kijani kibichi ni rangi inayowakilisha rotuba ya ardhi yetu na rangi nyeusi ni ya ngozi zetu.
Tatu: Aha! Ninafurahi kwamba unafahamu hayo.
Sironi: Ndiyo wajibu wetu haswa.
Tatu: Ninakubaliana nawe.
(Wanakimbia kuelekea darasani.)
© africaexams.com
Question : 3
Total: 30
Go to Question:
Advertisements