Test Index

KPSEA Kiswahili 2024 Paper

Show Para  Hide Para 
Question Numbers: 6-9
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Tulikuwa tumetulia tuli darasani kengele ilipokirizwa ghafla. Mara, kiranja wa darasa letu akatuambia kwamba tulikuwa tunahitajika kwenye ukumbi wa shule. Bila kupoteza muda tulifululiza hadi ukumbini na kuketi. Muda si muda. Mwalimu Mkuu, aliingia.
“Hamjambo nyote?” Mwalimu Mkuu alituamkua nasi tukamjibu kwa pamoja. Aliendelea, “Habari zinazotufikia sasa ni kuwa kuna mkurupuko wa ugonjwa hatari wa kipindupindu katika kata yetu ya Upendo. Inasemekana kuwa tayari ugonjwa huu umeathiri watu wengi wakiwemo watoto wa shule. Hii ndiyo maana tumekusanyika humu ili tujifahamishe kuhusu ugonjwa huu.
Ugonjwa wa kipindupindu unaweza kusababishwa na mambo mbalimbali. Inaaminika kwamba maji machafu yakichanganyika na maji safi ya kunywa na kupikia chakula huweza kusababisha kipindupindu. Taka zinazotupwa ovyo huwa makazi ya wadudu kama vile nzi ambao husambaza ugonjwa huu. Vilevile, kutozingatia usafi wakati wa kuandaa vyakula na vinywaji kunaweza kurahisisha uenezaji wa kipindupindu.
Ni jambo la busara kuhakikisha kwamba maji machafu hayapati njia ya kuchanganyika na maji safi yanayotumiwa na binadamu. Tunastahili kuwa na mapipa au mahali maalumu pa kutupa taka na kuzichoma. Tukumbuke kudumisha usafi kila mara tunapotayarisha chakula. Aidha, tunawe mikono kwa maji safi na sabuni na kwa njia inayofaa. Naomba tushirikiane kudumisha usafi ili kujiepusha na ugonjwa wa kipindupindu. Kama tunavyojua, kinga ni bora kuliko tiba. Ninawatakia siku njema!”
Sote tulimpigia Mwalimu Mkuu makofi kwa hotuba yake ya kuhamasisha kisha tukafumukana.
© africaexams.com
Question : 8
Total: 30
Go to Question:
Advertisements