Test Index

KPSEA Kiswahili 2025 Paper

Show Para  Hide Para 
Question Numbers: 13-15
Swali la 13 hadi la 15
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Baharini na maziwani mnaishi aina za samaki na wanyama wengine wengi. Wanyama hao wa majini wana umuhimu mkubwa kwa maisha ya binadamu kwa jumla. Kuna wale wanaotumiwa kama chakula, wanaosawazisha mazingira na hata wanaoipamba dunia tu. Kuna aina kadha za wanyama wa majini kama vile papa, nyangumi, dagaa na kambare. Bila kuwepo kwao binadamu atanyimwa sio tu chakula chenye madini bali pia burudani inayotokana na mienendo ya wanyama hao wawapo majini.
Baadhi ya wanyama wa majini ni wa ajabu. Mmoja wao ni papa. Papa anasemekana kwamba ndiye samaki mkubwa zaidi ulimwenguni. Ana ngozi ngumu, meno makubwa na hula watu! Wasemao husema ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Ikiwa umeshangazwa na ya papa kuwala watu, sikiliza ya nyangumi. Nyangumi ni mwenye kimo kikubwa. Utafiti unaonyesha kwamba anaweza kuwa na urefu wa futi tisini na uzani wa kilo elfu mia moja na hamsini. Nyangumi hunyonyesha vikembe vyake. Mataifa yanafaa, kuhakikisha kwamba uhai wa baharini unatunzwa kabla mambo yaende segemnege.
© africaexams.com
Question : 14
Total: 30
Go to Question:
Advertisements