Test Index

KPSEA Kiswahili 2025 Paper

Show Para  Hide Para 
Question Numbers: 6-9
Swali la 6 hadi la 9
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Daudi alipenda sana kucheza kandanda. Kila alipouona mchezo huo ukichezwa karibu naye alifululiza hadi pahali hapo na kuomba kushirikishwa. Wakati mwingine alijitengenezea mpira kwa vitambaa vikuukuu na kuwaita wenzake wacheze pamoja.
Siku moja, Daudi alitumwa dukani kununua mkate na pakiti ya maziwa. Alipokuwa akirudi nyumbani, aliona marafiki wake wakicheza kandanda karibu na nyumbani kwao. Ghafla, kiu yake ya kandanda iliamka, akasahau mfuko wa bidhaa aliokuwa amebeba na kujitoma katika mchezo. Yeye na wenzake walizama katika kusakata gozi. Hakuna aliyemwona paka akinyemelea mfuko ambao Daudi alikuwa ameuweka karibu na lango.
Daudi hakujua vipi, lakini baada ya muda, moyo ulimwambia autazame ule mfuko. Lo! Alimwona paka mkubwa ameining’iniza pakiti ya maziwa mdomoni. Daudi alitoka shoti kumfuata paka. Hata alipomfikia, pakiti ilikuwa tupu! Paka alikuwa amekamilisha kazi yake.
© africaexams.com
Question : 7
Total: 30
Go to Question:
Advertisements