Test Index
KPSEA Kiswahili 2026 Paper
Show Para
Question Numbers: 13-15Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.Michezo ni muhimu katika maisha ya binadamu. Tangu zamani binadamu amekuwa akishiriki katika michezo mbalimbali. Michezo yenyewe ni kama vile kandanda, netiboli, kuogelea na mbio. Kila mtu ana mchezo ambao anapenda kuucheza au kuushabikia.Kila mchezo una faida. Kuna michezo ambayo huburudisha. Unaposhiriki katika michezo kama hiyo, mwili huchangamka na akili hutulia. Aidha, michezo hutuletea kicheko na furaha isiyo na kifani. Hali kadhalika, michezo itakuwezesha kutumia muda wako vizuri na kukwepa kuingia kwenye tabia mbovu. Yaani, ukitumia wakati wako wa ziada kwenye michezo utaepuka marafiki wabaya. Mbali na faida hizo, michezo huwaleta pamoja watu wa taifa moja au mataifa mbalimbali.Sote tuna uwezo wa kushiriki katika mchezo fulani. Hivyo basi ni jukumu la kila mmoja wetu kutambua mchezo anaoupenda na kushiriki kikamilifu. Kwa kufanya hivyo, tutaimarisha afya yetu. Kumbuka pia, michezo inaweza kukupatia ajira katika siku zijazo.
Go to Question: