Test Index

KPSEA Kiswahili 2026 Paper

Show Para  Hide Para 
Question Numbers: 6-9
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Siku moja, Kantu alisahau kufunga dirisha la chumba chake alipotoka kuelekea shuleni. Aliporejea nyumbani jioni, alishangaa kumpata njiwa kitandani mwake.
“Huyu ni mmoja wa wale njiwa wanaoruka karibu na nyumba yetu. Nitamjengea kiota humu chumbani aishi nami.” Kantu alijisemea. Alimfungia yule njiwa chumbani mwake, akaenda kumwarifu rafiki yake Keshi, kuhusu tukio hilo.
“Nimepata njiwa katika chumba changu. Ningependa kumjengea kiota. Njoo unisaidie kukijenga,” Kantu alimwambia Keshi.
“Ni sawa. Twende nikamuone njiwa huyo kwanza.” Kantu aliandamana na Keshi hadi chumbani mwake.
“Ala! Ndiye huyu? Anapendeza kweli ila amejawa na woga. Lakini unafahamu kuwa hustahili kumfungia? Njiwa huyu anahitaji uhuru wake kama ndege wengine,” Keshi alimwambia Kantu.
“Kwa hivyo nifanye nini?” Kantu alimuuliza Keshi.
“Itabidi umwachilie. Huenda akajijengea kiota chake hapa nyumbani. Kwa njia hiyo, utafanya urafiki naye pasipo kumfungia.”
Kantu alijawa na mawazo. Baada ya muda, akamjibu Keshi.
“Nina huzuni kumwachilia aende lakini nimekuelewa. Ahsante sana Keshi kwa kunielimisha.” Kantu alisema, kisha akamuaga Keshi.
© africaexams.com
Question : 8
Total: 30
Go to Question:
Advertisements