Test Index
KPSEA Kiswahili 2025 Paper
Show Para
Question Numbers: 1-5Swali la 1 hadi la 5Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.(Ni jioni, shuleni. Maria ameketi kwenye fomu akisoma hadithi. Sara, rafikiye, anamjia kwa kunyatia.)Sara: (Baada ya kumwamkua.) Maria, ni hadithi gani hiyo ambayo imeyateka nyara mawazo yako mpaka huoni mvua ikija?Maria: (Akitabasamu.) Hata si hadithi. Ni yaliyomo katika hadithi yenyewe. Yanakuvuta tu bila kutaka.Sara: (Akimakinika zaidi.) Kwani inahusu nini?Maria: Inahusu jinsi urafiki wa Kuku na Mwewe ulivyofikia kikomo. (Akicheka.) Ni hali ya kusisimua na hapo hapo kuhuzunisha.Sara: (Akikubaliana naye.) Ahaa! Sasa naelewa sababu ya kuzama huko hadithini. Hata mimi ningependa kuisoma ila naona mvua ya masika inatishia kuanguka. Ni muhimu tuondoke.Maria: Kumbe! Sikuwa nimeona dalili ya mvua. Kweli, tunaweza kuondoka.
© africaexams.com
Question : 4
Total: 30
Go to Question: