Test Index

KPSEA Kiswahili 2025 Paper

Show Para  Hide Para 
Question Numbers: 1-5
Swali la 1 hadi la 5
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
(Ni jioni, shuleni. Maria ameketi kwenye fomu akisoma hadithi. Sara, rafikiye, anamjia kwa kunyatia.)
Sara: (Baada ya kumwamkua.) Maria, ni hadithi gani hiyo ambayo imeyateka nyara mawazo yako mpaka huoni mvua ikija?
Maria: (Akitabasamu.) Hata si hadithi. Ni yaliyomo katika hadithi yenyewe. Yanakuvuta tu bila kutaka.
Sara: (Akimakinika zaidi.) Kwani inahusu nini?
Maria: Inahusu jinsi urafiki wa Kuku na Mwewe ulivyofikia kikomo. (Akicheka.) Ni hali ya kusisimua na hapo hapo kuhuzunisha.
Sara: (Akikubaliana naye.) Ahaa! Sasa naelewa sababu ya kuzama huko hadithini. Hata mimi ningependa kuisoma ila naona mvua ya masika inatishia kuanguka. Ni muhimu tuondoke.
Maria: Kumbe! Sikuwa nimeona dalili ya mvua. Kweli, tunaweza kuondoka.
© africaexams.com
Question : 5
Total: 30
Go to Question:
Advertisements